Zaburi 37:1-4
Zaburi 37:1-4 NENO
Usisumbuke kwa ajili ya watendao maovu, wala usiwaonee wivu watendao mabaya, kwa maana watanyauka upesi kama majani, watakufa upesi kama mimea ya kijani. Mtumaini Mwenyezi Mungu na utende yaliyo mema. Kaa katika nchi ukafurahie malisho salama. Jifurahishe katika Mwenyezi Mungu naye atakupa haja za moyo wako.