Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 32:6-11

Zaburi 32:6-11 NENO

Kwa hiyo kila mtu mcha Mungu akuombe wakati unapopatikana, hakika maji makuu yatakapofurika hayatamfikia yeye. Wewe ndiwe mahali pangu pa kujificha, utaniepusha na taabu na kunizunguka kwa nyimbo za wokovu. Nitakufundisha na kukuonesha njia utakayoiendea; nitakushauri na kukuangalia. Usiwe kama farasi au nyumbu wasio na akili, ambao ni lazima waongozwe kwa lijamu na hatamu la sivyo hawatakukaribia. Mtu mwovu ana taabu nyingi, bali upendo usio na kikomo wa Mwenyezi Mungu unamzunguka mtu anayemtumaini. Shangilieni katika Mwenyezi Mungu na mfurahi, enyi wenye haki! Imbeni, nyote mlio wanyofu wa moyo!