Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 30:2-5

Zaburi 30:2-5 NENO

Ee Mwenyezi Mungu, Mungu wangu, nilikuita unisaidie na wewe umeniponya. Ee Mwenyezi Mungu, umenitoa Kuzimu, umeniokoa nisishuke kwenye shimo la mauti. Mwimbieni Mwenyezi Mungu, enyi watakatifu wake; lisifuni jina lake takatifu. Kwa maana hasira yake ni ya muda mfupi, bali upendo wake hudumu siku zote. Inawezekana kilio kiwepo usiku kucha, lakini furaha huja asubuhi.