Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 27:4-9

Zaburi 27:4-9 NENO

Jambo moja ninamwomba Mwenyezi Mungu, hili ndilo ninalolitafuta: niweze kukaa nyumbani mwa Mwenyezi Mungu siku zote za maisha yangu, niutazame uzuri wa Mwenyezi Mungu na kumtafuta hekaluni mwake. Kwa kuwa siku ya shida, atanihifadhi salama katika maskani yake, atanificha uvulini mwa hema lake, na kuniweka juu kwenye mwamba. Kisha kichwa changu kitainuliwa juu ya adui zangu wanaonizunguka. Katika maskani yake nitatoa dhabihu kwa kelele za shangwe; nitamwimbia Mwenyezi Mungu na kumsifu. Isikie sauti yangu nikuitapo, Ee Mwenyezi Mungu, unihurumie na unijibu. Moyo wangu unasema kuhusu wewe, “Utafute uso wake!” Uso wako, Mwenyezi Mungu “Nitautafuta.” Usinifiche uso wako, usimkatae mtumishi wako kwa hasira; wewe umekuwa msaada wangu. Usinikatae wala usiniache, Ee Mungu Mwokozi wangu.