Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 2:1-6

Zaburi 2:1-6 NEN

Kwa nini mataifa wanashauriana kufanya mabaya, na kabila za watu kula njama bure? Wafalme wa dunia wanajipanga na watawala wanajikusanya pamoja dhidi ya BWANA na dhidi ya Mpakwa Mafuta wake. Wanasema, “Tuvunje minyororo yao na kuvitupilia mbali vifungo vyao.” Yeye atawalaye mbinguni hucheka, Bwana huwadharau. Kisha huwakemea katika hasira yake na kuwaogopesha katika ghadhabu yake, akisema, “Nimemtawaza Mfalme wangu juu ya Sayuni, mlima wangu mtakatifu.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 2:1-6