Zaburi 18:32-34
Zaburi 18:32-34 NEN
Mungu ndiye anivikaye nguvu na kufanya njia yangu kuwa kamilifu. Huifanya miguu yangu kama miguu ya kulungu, huniwezesha kusimama mahali palipo juu. Huifundisha mikono yangu kupigana vita; mikono yangu inaweza kupinda upinde wa shaba.