Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 140

140
Zaburi 140
Kuomba Ulinzi Wa Mungu
Kwa mwimbishaji. Zaburi ya Daudi.
1 Ee Bwana, niokoe, kutoka kwa watu waovu;
nilinde na watu wenye jeuri,
2 ambao hupanga mipango mibaya mioyoni mwao,
na kuchochea vita siku zote.
3 Wao hufanya ndimi zao kali kama za nyoka,
sumu ya nyoka iko midomoni mwao.
4 Ee Bwana, niepushe na mikono ya waovu;
nilinde na watu wenye jeuri
wanaopanga kunikwaza miguu yangu.
5 Wenye kiburi wameficha mtego wa kuninasa,
wametandaza kamba za wavu wao,
wametega mitego kwenye njia yangu.
6 Ee Bwana, ninakuambia, “Wewe ni Mungu wangu.”
Ee Bwana, usikie kilio changu na kunihurumia.
7Ee Bwana Mwenyezi, Mwokozi wangu mwenye nguvu,
unikingaye kichwa changu siku ya vita:
8 Ee Bwana, usiwape waovu matakwa yao,
usiache mipango yao ikafanikiwa,
wasije wakajisifu.
9 Vichwa vya wanaonizunguka vifunikwe
na shida zinazosababishwa na midomo yao.
10 Makaa ya mawe ya moto na yawaangukie!
Na watupwe motoni,
katika mashimo ya matope,
wasiinuke tena kamwe.
11 Wasingiziaji wasifanikiwe katika nchi;
maafa na yawawinde watu wenye jeuri.
12 Najua kwamba Bwana huwapatia maskini haki,
na kuitegemeza njia ya mhitaji.
13 Hakika wenye haki watalisifu jina lako,
na waadilifu wataishi mbele zako.

Iliyochaguliwa sasa

Zaburi 140: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha