Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 139:16-24

Zaburi 139:16-24 NEN

macho yako yaliniona kabla mwili wangu haujakamilika. Siku zangu zote ulizonipangia ziliandikwa katika kitabu chako kabla haijakuwepo hata moja. Tazama jinsi yalivyo ya thamani mawazo yako kwangu, Ee Mungu! Jinsi jumla yake ilivyo kubwa! Kama ningezihesabu, zingekuwa nyingi kuliko mchanga. Niamkapo, bado niko pamoja nawe. Laiti ungewachinja waovu, Ee Mungu! Ondokeni kwangu, ninyi wamwaga damu! Wanazungumza juu yako wakiwa na kusudi baya, adui zako wanatumia vibaya jina lako. Ee BWANA, je, nisiwachukie wanaokuchukia? Nisiwachukie sana wanaoinuka dhidi yako? Sina kitu zaidi ya chuki dhidi yao, ninawahesabu ni adui zangu. Ee Mungu, nichunguze, uujue moyo wangu, nijaribu na ujue mawazo yangu. Uone kama kuna njia iletayo machukizo ndani yangu, uniongoze katika njia ya milele.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 139:16-24