Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 135:1-5

Zaburi 135:1-5 NEN

Msifuni BWANA. Lisifuni jina la BWANA, msifuni, enyi watumishi wa BWANA, ninyi ambao mnatumika ndani ya nyumba ya BWANA, katika nyua za nyumba ya Mungu wetu. Msifuni BWANA, kwa kuwa BWANA ni mwema, liimbieni sifa jina lake, kwa maana hilo lapendeza. Kwa maana BWANA amemchagua Yakobo kuwa wake mwenyewe, Israeli kuwa mali yake ya thamani. Ninajua ya kuwa BWANA ni mkuu, kwamba Bwana wetu ni mkuu kuliko miungu yote.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 135:1-5