Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 133:1-3

Zaburi 133:1-3 NEN

Tazama jinsi ilivyo vyema na kupendeza wakati ndugu wanapoishi pamoja katika umoja! Ni kama mafuta ya thamani yaliyomiminwa kichwani, yakitiririka kwenye ndevu, yakitiririka kwenye ndevu za Aroni, mpaka kwenye upindo wa mavazi yake. Ni kama vile umande wa Hermoni unavyoanguka juu ya Mlima Sayuni. Kwa maana huko ndiko BWANA alikoamuru baraka yake, naam, hata uzima milele.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Zaburi 133:1-3