Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Zaburi 103:1-5

Zaburi 103:1-5 NEN

Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA. Vyote vilivyomo ndani yangu vilihimidi jina lake takatifu. Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, wala usisahau wema wake wote, akusamehe dhambi zako zote, akuponya magonjwa yako yote, aukomboa uhai wako na kaburi, akuvika taji ya upendo na huruma, atosheleza mahitaji yako kwa vitu vyema, ili ujana wako uhuishwe kama wa tai.