Mithali 3:21-24
Mithali 3:21-24 NEN
Mwanangu, hifadhi maamuzi mema na busara, usiache vitoke machoni pako; ndipo vitakapokuwa uzima nafsini mwako na pambo la neema shingoni mwako. Kisha utaenda katika njia yako salama, wala mguu wako hautajikwaa; ulalapo, hautaogopa; ulalapo usingizi wako utakuwa mtamu.