Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mithali 20:1-15

Mithali 20:1-15 NENO

Mvinyo ni mdhihaki na kileo ni mgomvi; yeyote apotoshwaye navyo hana hekima. Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; yeye amkasirishaye hupoteza uhai wake. Ni kwa heshima ya mtu kujitenga ugomvi, bali kila mpumbavu ni mwepesi kugombana. Mvivu halimi kwa majira; kwa hiyo wakati wa mavuno hutazama lakini hapati chochote. Makusudi ya moyo wa mwanadamu ni maji yenye kina, lakini mtu mwenye ufahamu huyachota. Watu wengi hujidai kuwa na upendo usiokoma, bali mtu mwaminifu ni nani awezaye kumpata? Mtu mwenye haki huishi maisha yasiyo na lawama, wamebarikiwa watoto wake baada yake. Mfalme anapoketi kwenye kiti chake cha ufalme kuhukumu, hupepeta ubaya wote kwa macho yake. Ni nani awezaye kusema, “Nimeuweka moyo wangu safi; mimi ni safi na sina dhambi?” Mawe ya kupimia yaliyo tofauti na vipimo tofauti, Mwenyezi Mungu huchukia vyote viwili. Hata mtoto hujulikana kwa matendo yake, kama tabia yake ni safi na adili. Masikio yasikiayo na macho yaonayo: Mwenyezi Mungu ndiye alivifanya vyote viwili. Usiupende usingizi la sivyo utakuwa maskini, uwe macho nawe utakuwa na chakula cha akiba. “Haifai, haifai!” asema mnunuzi, kisha huondoka akijisifia ununuzi wake. Kuna dhahabu, na marijani kwa wingi, lakini midomo inayonena maarifa ni kito cha thamani.