Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 33

33
Vituo katika safari ya Waisraeli
1Hivi ndivyo vituo katika safari ya Waisraeli walipotoka Misri kwa vikosi chini ya uongozi wa Musa na Haruni. 2Kwa agizo la Mwenyezi Mungu, Musa aliweka kumbukumbu ya vituo katika safari yao. Hivi ndivyo vituo katika safari yao:
3Waisraeli walisafiri kutoka Ramesesi katika siku ya kumi na tano ya mwezi wa kwanza, siku iliyofuata Pasaka. Walitembea kwa ujasiri wazi mbele ya Wamisri wote, 4waliokuwa wakizika wazaliwa wao wa kwanza wote, ambao Mwenyezi Mungu alikuwa amewaua kati yao, kwa kuwa Mwenyezi Mungu alikuwa ameleta hukumu juu ya miungu yao.
5Waisraeli waliondoka Ramesesi na kupiga kambi huko Sukothi.
6Wakaondoka Sukothi na kupiga kambi huko Ethamu, pembeni mwa jangwa.
7Wakaondoka Ethamu, wakageuka wakarudi Pi-Hahirothi, hadi mashariki mwa Baal-Sefoni, wakapiga kambi yao karibu na Migdoli.
8Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari hadi jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara.
9Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi.
10Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu.
11Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini.
12Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka.
13Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi.
14Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji ya watu kunywa.
15Wakaondoka Refidimu na kupiga kambi katika Jangwa la Sinai.
16Wakaondoka katika Jangwa la Sinai na kupiga kambi huko Kibroth-Hataava.
17Wakaondoka Kibroth-Hataava na kupiga kambi huko Haserothi.
18Wakaondoka Haserothi na kupiga kambi huko Rithma.
19Wakaondoka Rithma na kupiga kambi huko Rimon-Peresi.
20Wakaondoka Rimon-Peresi na kupiga kambi huko Libna.
21Wakaondoka Libna na kupiga kambi huko Risa.
22Wakaondoka Risa na kupiga kambi huko Kehelatha.
23Wakaondoka Kehelatha na kupiga kambi kwenye mlima Sheferi.
24Wakaondoka kwenye mlima Sheferi na kupiga kambi huko Harada.
25Wakaondoka Harada na kupiga kambi huko Makelothi.
26Wakaondoka Makelothi na kupiga kambi huko Tahathi.
27Wakaondoka Tahathi na kupiga kambi huko Tera.
28Wakaondoka Tera na kupiga kambi huko Mithka.
29Wakaondoka Mithka na kupiga kambi huko Hashmona.
30Wakaondoka Hashmona na kupiga kambi Moserothi.
31Wakaondoka Moserothi na kupiga kambi huko Bene-Yaakani.
32Wakaondoka Bene-Yaakani na kupiga kambi huko Hor-Hagidgadi.
33Wakaondoka Hor-Hagidgadi na kupiga kambi huko Yotbatha.
34Wakaondoka Yotbatha na kupiga kambi huko Abrona.
35Wakaondoka Abrona na kupiga kambi huko Esion-Geberi.
36Wakaondoka Esion-Geberi na kupiga kambi huko Kadeshi katika Jangwa la Sini.
37Wakaondoka Kadeshi na kupiga kambi kwenye Mlima Hori, mpakani mwa Edomu. 38Kwa amri ya Mwenyezi Mungu, kuhani Haruni alipanda Mlima Hori, mahali alipofia katika siku ya kwanza ya mwezi wa tano, mwaka wa arobaini baada ya Waisraeli kutoka Misri. 39Haruni alikufa juu ya Mlima Hori akiwa na umri wa miaka mia moja ishirini na tatu (123).
40Mfalme Mkanaani wa Aradi, ambaye aliishi huko Negebu ya Kanaani, akasikia kwamba Waisraeli wanakuja.
41Wakaondoka kwenye mlima Hori na kupiga kambi huko Salmona.
42Wakaondoka Salmona, wakapiga kambi huko Punoni.
43Wakaondoka Punoni, wakapiga kambi huko Obothi.
44Wakaondoka Obothi, wakapiga kambi huko Iye-Abarimu, mipakani mwa Moabu.
45Wakaondoka Iye-Abarimu, wakapiga kambi huko Dibon-Gadi.
46Wakaondoka Dibon-Gadi na kupiga kambi huko Almon-Diblathaimu.
47Wakaondoka Almon-Diblathaimu na kupiga kambi katika milima ya Abarimu, karibu na Nebo.
48Wakaondoka kwenye milima ya Abarimu na kupiga kambi kwenye tambarare ya Moabu, kando ya Yordani, ng’ambo ya Yeriko. 49Huko kwenye tambarare za Moabu walipiga kambi kandokando ya Mto Yordani, kuanzia Beth-Yeshimothi hadi Abel-Shitimu.
50Katika tambarare za Moabu kando ya Yordani, ng’ambo ya Yeriko, Mwenyezi Mungu akamwambia Musa, 51“Sema na Waisraeli uwaambie: ‘Mtakapovuka Mto Yordani kuingia Kanaani, 52wafukuzeni wakazi wote wa nchi iliyo mbele yenu. Haribuni sanamu zao zote za kuchongwa, na sanamu zilizotengenezwa kwa kusubu, na kubomoa mahali pao pa juu pa kuabudia. 53Mtaimiliki nchi hiyo na kukaa huko, kwa kuwa nimewapeni ninyi kuimiliki. 54Mtaigawanya nchi hiyo kwa kupiga kura, kufuatana na koo zenu. Kwa kundi kubwa zaidi toa urithi mkubwa zaidi, na kwa kundi dogo zaidi urithi mdogo zaidi. Chochote kinachowaangukia kwa kura kitakuwa chao. Mtaigawanya nchi kufuatana na makabila ya babu zenu.
55“ ‘Lakini kama hamkuwafukuza wenyeji wa nchi hiyo, wale mtakaowaruhusu wabaki watakuwa kama sindano kwenye macho yenu na miiba kwenu kila upande. Watawasumbua katika nchi mtakayoishi. 56Kisha nitawatenda ninyi kile ambacho nimepanga kuwatenda wao.’ ”

Iliyochaguliwa sasa

Hesabu 33: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia