Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hesabu 33:8-14

Hesabu 33:8-14 NEN

Wakaondoka Pi-Hahirothi wakapita katikati ya bahari mpaka jangwani, na baada ya kusafiri kwa siku tatu katika Jangwa la Ethamu, walipiga kambi huko Mara. Wakaondoka Mara wakaenda Elimu, mahali ambapo palikuwa na chemchemi kumi na mbili na mitende sabini, huko wakapiga kambi. Wakaondoka Elimu na kupiga kambi kando ya Bahari ya Shamu. Wakaondoka kando ya Bahari ya Shamu na kupiga kambi katika Jangwa la Sini. Wakaondoka katika Jangwa la Sini, wakapiga kambi huko Dofka. Wakaondoka Dofka, wakapiga kambi huko Alushi. Wakaondoka Alushi, wakapiga kambi Refidimu, mahali ambapo hapakuwa na maji kwa ajili ya watu kunywa.

Video for Hesabu 33:8-14