Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Nahumu Utangulizi

Utangulizi
Jina “Nahumu” maana yake ni “Faraja”. Nahumu alikuwa raia wa Elkoshi na alihudumu wakati mmoja na Sefania, Yeremia na Habakuki. Katika ujumbe wake alizungumzia kuanguka kwa Thebesi mwaka wa 663 K.K. na kuanguka kwa Ninawi mnamo mwaka wa 612 K.K. Ninawi, mji mkuu wa Ashuru, ulikuwa ni alama ya ukatili, mateso, hali ya kujilimbikizia mali, na utawala wa nguvu. Hii ndiyo sababu mji huu uliangushwa mwaka 621 K.K. Miaka michache kabla ya kuangushwa kwa mji wa Ninawi, Nabii Nahumu alitabiri kuhusu tukio hilo.
Kitabu hiki kimehifadhi ujumbe mfupi wa Nahumu juu ya Ninawi. Katika unabii huu Nahumu anaelezea na kuonesha kuzingirwa na kuanguka kwa Ninawi kuwa ndio mwisho wa ufalme huu wa Ashuru. Kwa mantiki hiyo, Nahumu anawashauri watu wake kuzitii sikukuu zao za kidini, kwa kuwa Waashuru wasingeushambulia mji wa Yerusalemu tena. Ingawa ujumbe unaonesha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Ninawi, ni muhimu sana ujumbe huu ukachukuliwa sambamba na ujumbe wa Nabii Yona kwamba Mwenyezi Mungu aliupenda mji wa Ninawi.
Mwandishi
Nahumu.
Kusudi
Kutangaza hukumu ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Waashuru na kutoa ujumbe wa faraja kwa watu wa Yuda.
Mahali
Ninawi.
Tarehe
Mnamo 663–612 K.K.
Wahusika Wakuu
Watu wa Ninawi na Waisraeli.
Wazo Kuu
Kuangamizwa kwa Ninawi na faraja kwa Waisraeli.
Mambo Muhimu
Nahumu anaeleza kukaribia kwa hukumu ya Ninawi na jinsi itakavyokuwa kwa lugha ya wazi. Anaorodhesha kwa kifupi dhambi za Ninawi na kutamka kwamba Mwenyezi Mungu ni mwenye haki katika hukumu zake. Anamalizia kwa kuiona hukumu iliyokamilika. Hiki ndicho kitabu cha Manabii kinachotoa unabii wake waziwazi juu ya ukatili wa Waashuru.
Yaliyomo
Hasira ya Mwenyezi Mungu dhidi ya Ninawi (1:1-15)
Kuanguka kwa Ninawi (2:1-13)
Ole wa Ninawi (3:1-19).

Iliyochaguliwa sasa

Nahumu Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia