Marko 6:37-38
Marko 6:37-38 NENO
Lakini Yesu akawajibu, “Ninyi wapeni chakula.” Wakamwambia, “Je, twende tukanunue mikate ya dinari mia mbili ili tuwape watu hawa wale?” Akawauliza, “Kuna mikate mingapi? Nendeni mkaangalie.” Walipokwisha kujua, wakarudi, wakamwambia, “Kuna mikate mitano na samaki wawili.”