Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mika 7:6-8

Mika 7:6-8 NEN

Kwa kuwa mwana humdharau baba yake, naye binti huinuka dhidi ya mama yake, mkwe kuwa kinyume na mama mkwe wake: adui wa mtu ni wale wa nyumbani mwake hasa. Lakini mimi, namtazama BWANA kwa matumaini, namngoja Mungu Mwokozi wangu; Mungu wangu atanisikia mimi. Usifurahie msiba wangu, ee adui yangu! Ingawa nimeanguka, nitainuka. Japo ninaketi gizani, BWANA atakuwa nuru yangu.