Mathayo 9:27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37
Mathayo 9:27 NENO
Isa alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipaza sauti na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!”
Mathayo 9:28 NENO
Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Isa akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?” Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.”
Mathayo 9:29 NENO
Ndipo Isa akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.”
Mathayo 9:30 NENO
Macho yao yakafunguka. Isa akawaonya vikali, akisema, “Chungeni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.”
Mathayo 9:31 NENO
Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.
Mathayo 9:32 NENO
Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Isa.
Mathayo 9:33 NENO
Yule pepo mchafu alipotolewa, yule mtu aliyekuwa bubu akaongea, na umati wa watu wakastaajabu na kusema, “Jambo kama hili kamwe halijapata kuonekana katika Israeli.”
Mathayo 9:34 NENO
Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa mkuu wa pepo wachafu.”
Mathayo 9:35 NENO
Isa akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri Habari Njema za ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi.
Mathayo 9:36 NENO
Alipoona umati wa watu, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.
Mathayo 9:37 NENO
Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache.