Mathayo 9:27, 28, 29, 30, 31, 32, 33, 34, 35, 36, 37
Mathayo 9:27 NEN
Yesu alipokuwa akiondoka mahali pale, vipofu wawili wakamfuata wakipiga kelele kwa nguvu na kusema, “Mwana wa Daudi, tuhurumie!”
Mathayo 9:28 NEN
Alipoingia mle nyumbani wale vipofu wakamjia. Naye Yesu akawauliza, “Mnaamini kwamba ninaweza kufanya jambo hili?” Wakamjibu, “Ndiyo, Bwana.”
Mathayo 9:29 NEN
Ndipo Yesu akagusa macho yao na kusema, “Iwe kwenu sawasawa na imani yenu.”
Mathayo 9:30 NEN
Macho yao yakafunguka. Yesu akawaonya vikali, akisema, “Angalieni mtu yeyote asijue kuhusu jambo hili.”
Mathayo 9:31 NEN
Lakini wao wakaenda na kueneza habari zake katika eneo lile lote.
Mathayo 9:32 NEN
Walipokuwa wanatoka, mtu mmoja aliyekuwa amepagawa na pepo mchafu na ambaye hakuweza kuongea aliletwa kwa Yesu.
Mathayo 9:33 NEN
Yule pepo mchafu alipotolewa, yule mtu aliyekuwa bubu akaongea. Ule umati wa watu ukastaajabu na kusema, “Jambo kama hili kamwe halijapata kuonekana katika Israeli.”
Mathayo 9:34 NEN
Lakini Mafarisayo wakasema, “Huyo anatoa pepo wachafu kwa uwezo wa mkuu wa pepo wachafu.”
Mathayo 9:35 NEN
Yesu akazunguka katika miji yote na vijiji vyote, akifundisha katika masinagogi yao, akihubiri habari njema za Ufalme, na akiponya kila ugonjwa na kila aina ya maradhi.
Mathayo 9:36 NEN
Alipoona makutano, aliwahurumia kwa sababu walikuwa wanasumbuka bila msaada, kama kondoo wasiokuwa na mchungaji.
Mathayo 9:37 NEN
Ndipo akawaambia wanafunzi wake, “Mavuno ni mengi lakini watendakazi ni wachache.