Mathayo 12:46-50
Mathayo 12:46-50 NENO
Wakati alikuwa angali anazungumza na umati wa watu, mama yake na ndugu zake wakasimama nje wakitaka kuongea naye. Ndipo mtu mmoja akamwambia, “Tazama, mama yako na ndugu zako wamesimama nje, wanataka kuongea na wewe.” Lakini yeye akamjibu na kumwambia yule mtu, “Mama yangu ni nani, nao ndugu zangu ni nani?” Akawanyooshea mkono wanafunzi wake, akasema, “Hawa hapa ndio mama yangu na ndugu zangu! Kwa maana yeyote afanyaye mapenzi ya Baba yangu wa mbinguni, huyo ndiye kaka yangu, na dada yangu, na mama yangu.”