Mathayo 12:15-21
Mathayo 12:15-21 NEN
Lakini Yesu alipoyatambua mawazo yao, akaondoka mahali hapo. Watu wengi wakamfuata, naye akawaponya wagonjwa wao wote, akiwakataza wasiseme yeye ni nani. Hii ilikuwa ili litimie lile neno lililonenwa kwa kinywa cha nabii Isaya kusema: “Tazama mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu, ninayependezwa naye. Nitaweka Roho wangu juu yake, naye atatangaza haki kwa mataifa. Hatagombana wala hatapiga kelele, wala hakuna atakayesikia sauti yake njiani. Mwanzi uliopondeka hatauvunja, na utambi unaofuka moshi hatauzima, mpaka atakapoifanya haki ishinde. Katika Jina lake mataifa wataweka tumaini lao.”