Mathayo 1:18-24
Mathayo 1:18-24 NENO
Kuzaliwa kwake Isa Al-Masihi kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa ameposwa na Yusufu, lakini kabla hawajakutana kimwili, Mariamu alionekana kuwa na mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu wa Mungu. Kwa kuwa Yusufu, mwanaume aliyekuwa amemposa alikuwa mtu mwadilifu, hakutaka kumwaibisha Mariamu hadharani, hivyo basi alikusudia kumwacha kwa siri. Lakini alipokuwa akifikiri kufanya jambo hili, malaika wa Mwenyezi Mungu akamtokea katika ndoto na kusema, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako, kwa maana mimba aliyo nayo ni kwa uweza wa Roho wa Mungu. Naye atamzaa mwana, nawe utamwita jina Isa, kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka dhambi zao.” Haya yote yalitukia ili litimie lile Mwenyezi Mungu alilonena kupitia nabii, aliposema: “Tazama, bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, nao watamwita jina Imanueli” (maana yake, “Mungu pamoja nasi”). Yusufu alipoamka kutoka usingizini, akafanya jinsi alivyoagizwa na malaika wa Mwenyezi Mungu, akamchukua Mariamu kuwa mke wake.