Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Malaki 3:13-18

Malaki 3:13-18 NEN

“Mmesema vitu vigumu dhidi yangu,” asema BWANA. “Hata hivyo mnauliza, ‘Tumesema nini dhidi yako?’ “Mmesema, ‘Ni bure kumtumikia Mungu. Tumepata faida gani kwa kushika maagizo yake na kwenda kama waombolezaji mbele za BWANA Mwenye Nguvu Zote? Lakini sasa wenye kiburi wanabarikiwa. Hakika watenda mabaya wanastawi, pia hata wale wanaoshindana na Mungu ndio wanaosalimika.’ ” Ndipo wale waliomcha BWANA wakasemezana wao kwa wao, naye BWANA akasikiliza na akasikia. Kitabu cha kumbukumbu kikaandikwa mbele yake kuhusu wale ambao walimcha BWANA na kuliheshimu jina lake. “Nao watakuwa watu wangu,” asema BWANA Mwenye Nguvu Zote, “katika siku ile nitakapowafanya watu kuwa hazina yangu. Nitawahurumia, kama vile kwa huruma mtu amhurumiavyo mwanawe anayemtumikia. Kwa mara nyingine tena utaona tofauti kati ya wenye haki na waovu, kati ya wale wanaomtumikia Mungu na wale wasiomtumikia.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Malaki 3:13-18

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha