Luka Utangulizi
Utangulizi
Luka alikuwa tabibu. Utangulizi wa Injili ya Luka na ule wa Matendo ya Mitume zinaunganisha vitabu hivi pamoja. Vyote viliandikiwa mtu maarufu wa Kiyunani aliyeitwa Theofilo (maana yake ni Mpendwa wa Mungu). Lugha na mtindo wa Injili ya Luka na pia Matendo unaonesha kuwa alikuwa mtaalamu mwenye uwezo mkubwa wa kuandika kwa ufasaha, aliyekuwa na elimu ya juu, na asili na mtazamo wa Kiyunani.
Inaaminika kwamba Luka alikuwa mtu wa Mataifa aliyeokoka kutoka Antiokia ya Siria. Aliungana na Paulo huko Troa katika safari ya Paulo ya pili kueneza Injili. Ingawa kuna kazi nyingine nyingi kumhusu Kristo, Luka alitoa mpangilio na mtiririko wa matukio kama mwana-historia ambaye alikuwa na habari za kina, na mwenye uwezo wa kuandika na kutoa habari za kuaminika.
Mwandishi
Luka.
Kusudi
Kudhihirisha habari sahihi za maisha ya Kristo, na kuthibitisha kwamba Kristo ni Mungu na pia Mwanadamu mkamilifu aliyekuja duniani kwa huduma ya ukombozi wa mwanadamu.
Mahali
Rumi au Kaisaria.
Tarehe
Mnamo 60 B.K.
Wahusika Wakuu
Yesu na wanafunzi wake, Elizabeti na Zakaria, Yohana Mbatizaji na wanafunzi wake, Mariamu, Herode Mkuu, Pilato, na Mariamu Magdalene.
Wazo Kuu
Luka anaeleza asili ya Umasiya wa Yesu, na kusudi la huduma yake.
Mambo Muhimu
Luka anadhihirisha kazi na mafundisho ya Yesu, hasa kuelewa mpango wa wokovu, maombi ya Yesu, uhusiano wake na watu maskini na watu wa Mataifa waliotengwa na Wayahudi, na kudhihirisha kuhusu Roho Mtakatifu. Injili ya Luka ndiyo ndefu kuliko zote.
Yaliyomo
Utangulizi; kuzaliwa kwa Yesu na ujana wake (1:1–2:52)
Yohana Mbatizaji na Yesu, na kujaribiwa kwa Yesu (3:1–4:13)
Huduma ya Yesu huko Galilaya (4:14–9:50)
Safari ya Yesu kwenda Yerusalemu (9:51–19:44)
Huduma ya Yesu huko Yerusalemu (19:45–20:47)
Unabii kuhusu mambo yajayo (21:1‑38)
Kufa na kufufuka kwa Yesu (22:1–24:53).
Iliyochaguliwa sasa
Luka Utangulizi: NENO
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015, 2025 by Biblica, Inc.
Used with permission. All rights reserved worldwide.