Luka 6:24-27
Luka 6:24-27 NEN
“Lakini ole wenu ninyi mlio matajiri, kwa sababu mmekwisha kupokea faraja yenu. Ole wenu ninyi mlioshiba sasa, maana mtaona njaa. Ole wenu ninyi mnaocheka sasa, maana mtaomboleza na kulia. Ole wenu watu watakapowasifu, kwani ndivyo baba zao walivyowasifu manabii wa uongo. “Lakini nawaambia ninyi mnaonisikia: Wapendeni adui zenu. Watendeeni mema wanaowachukia.