Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 10:40-42

Luka 10:40-42 NEN

Lakini Martha alikuwa akihangaika na maandalizi yote yaliyokuwa yafanyike. Martha akaja kwa Yesu na kumuuliza, “Bwana, hujali kwamba ndugu yangu ameniachia kazi zote mwenyewe? Basi mwambie anisaidie.” Lakini Bwana akamjibu, “Martha, Martha, mbona unasumbuka na kuhangaika na mengi? Lakini kunahitajika kitu kimoja tu. Maria amechagua kile kilicho bora, wala hakuna mtu atakayemwondolea.”