Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Luka 1:46-55

Luka 1:46-55 NEN

Naye Maria akasema: “Moyo wangu wamwadhimisha Bwana, nayo roho yangu inamfurahia Mungu Mwokozi wangu, kwa kuwa ameangalia kwa fadhili unyonge wa mtumishi wake. Hakika tangu sasa vizazi vyote vitaniita aliyebarikiwa, kwa maana yeye Mwenye Nguvu amenitendea mambo ya ajabu: jina lake ni takatifu. Rehema zake huwaendea wale wamchao, kutoka kizazi hadi kizazi. Kwa kuwa ametenda mambo ya ajabu kwa mkono wake; amewatawanya wale wenye kiburi ndani ya mioyo yao. Amewashusha watawala toka kwenye viti vyao vya enzi, lakini amewainua wanyenyekevu. Amewashibisha wenye njaa kwa vitu vizuri, bali matajiri amewafukuza mikono mitupu. Amemsaidia mtumishi wake Israeli, kwa kukumbuka ahadi yake ya kumrehemu Abrahamu na uzao wake milele, kama alivyowaahidi baba zetu.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Luka 1:46-55