Walawi Utangulizi
Utangulizi
Kitabu cha Walawi kinajulikana kama “Kitabu cha Makuhani,” jina lililotokana na tafsiri ya Agano la Kale la Kiyunani. Walawi walichaguliwa na Mungu kuwa makuhani. Kitabu cha Walawi kina amri nyingi walizopaswa kuzitii na kuzitenda. Kazi ya ukuhani ilikuwa ya kushughulikia matatizo ya kila siku kuhusu uadilifu wa Waisraeli wote, jinsi ya kumwabudu Mungu, na kuishi katika utakatifu kama watu wateule wa Mungu.
Katika Agano la Kale, Mungu aliamuru kutolewa kwa sadaka na dhabihu, nazo zikapata maana kutokana na uhusiano wa Agano la Mungu na Israeli. Makusanyiko matakatifu yaliyofanyika katika mwaka yalitoa mwito kwa Waisraeli kufanya upya tabia na ile hali ya kutambua wajibu wao kama watu waliochaguliwa na Mungu. Ondoleo la dhambi lilifanyika kwa njia ya kumwaga damu wakati wanyama walipokuwa wanatolewa dhabihu, kufuatana na maelekezo yaliyokuwa yametolewa kupitia kwa Mose.
Mwandishi
Mose, kiongozi wa Israeli.
Kusudi
Kusudi la kitabu hiki ni kuonyesha kwa undani sheria zilizokuwa zinawaongoza Waisraeli, yaani makuhani pamoja na watu, katika Agano la uhusiano na Mungu.
Mahali
Chini ya Mlima Sinai, wakati wa safari ya wana wa Israeli.
Tarehe
Kati ya 1450–1410 K.K.
Wahusika Wakuu
Walawi, Mose, Aroni, Nadabu, Abihu, Eleazari na Ithamari.
Wazo Kuu
Kitabu hiki cha tatu miongoni mwa Vitabu Vitano vya Mose kinashughulika kwa msingi kuhusu kuishi maisha matakatifu na kumwabudu Mungu.
Mambo Muhimu
Utakatifu umetajwa mara nyingi katika kitabu hiki kuliko kitabu kingine chochote cha Biblia. Mungu anawafundisha Waisraeli jinsi ya kuishi maisha matakatifu: Mungu mtakatifu, ukuhani mtakatifu, watu watakatifu, dhabihu takatifu, vyombo vitakatifu, vyakula vitakatifu, pamoja na sheria ya utakatifu kwa ajili ya maisha ya utaua.
Mgawanyo
Amri na maelekezo ya kutoa dhabihu na sadaka (1:1–7:38)
Aroni na wanawe wateuliwa na Mungu kuwa makuhani (8:1–10:20)
Sheria zinazosimamia usafi na unajisi (11:1–15:33)
Siku ya Upatanisho (16:1-34)
Sheria za utakatifu kimatendo (17:1–22:33)
Sabato, sikukuu na majira (23:1–25:55)
Mambo ya kufanya ili kustahili baraka za Mungu (26:1–27:34).
Iliyochaguliwa sasa
Walawi Utangulizi: NEN
Kuonyesha
Shirikisha
Nakili
Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia
Neno: Biblia Takatifu™ Neno™
Hakimiliki © 1984, 1989, 2009, 2015 na Biblica, Inc.
Imetumiwa kwa ruhusa. Haki zote zimehifadhiwa duniani kote.
Kiswahili Contemporary Version™
Copyright © 1984, 1989, 2009, 2015 by Biblica, Inc.
Used with Permission. All Rights Reserved Worldwide.