Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yoshua 5:13-15

Yoshua 5:13-15 NEN

Basi wakati Yoshua alipokuwa karibu na Yeriko, akainua macho, akaona mtu aliyesimama mbele yake, akiwa na upanga mkononi uliofutwa kwenye ala. Yoshua akamwendea na kumuuliza, “Je, wewe uko upande wetu au upande wa adui zetu?” Akajibu, “La, siko upande wowote, lakini mimi nimekuja nikiwa jemadari wa jeshi la BWANA.” Yoshua akaanguka kifudifudi hadi chini, akasujudu, akamuuliza, “Je, Bwana, una ujumbe gani kwa mtumishi wako?” Jemadari wa jeshi la BWANA akajibu, “Vua viatu vyako, kwa maana mahali hapa unaposimama ni patakatifu.” Naye Yoshua akafanya hivyo.