Yoshua 10:12-14
Yoshua 10:12-14 NEN
Katika siku ile ambayo BWANA aliwapeana Waamori kwa Israeli, Yoshua akanena na BWANA akiwa mbele ya Waisraeli akasema: “Wewe jua, simama juu ya Gibeoni, wewe mwezi, tulia juu ya Bonde la Aiyaloni.” Hivyo jua likasimama, nao mwezi ukatulia, hadi taifa hilo lilipokwisha kujilipizia kisasi kwa adui wake, kama ilivyoandikwa katika Kitabu cha Yashari. Jua likasimama kimya katikati ya mbingu, likachelewa kuzama muda wa siku moja nzima. Haijakuwepo siku nyingine kama hiyo kabla au baada, siku ambayo BWANA alimsikiliza mwanadamu. Hakika BWANA alikuwa akiwapigania Israeli.