Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Ayubu 38:25-38

Ayubu 38:25-38 NENO

Ni nani aliyepasua mifereji kwa ajili ya maji mengi ya mvua yaendayo kasi na njia ya miali ya radi, ili kusababisha mvua kunyeshea mahali pasipokaliwa na mtu, jangwa lisilo na yeyote ndani yake, ili kuitosheleza nchi ya ukiwa na jangwa, na majani yaanze kumea ndani yake? Je, mvua ina baba? Ni nani baba azaaye matone ya umande? Barafu inatoka tumbo la nani? Ni nani azaaye ukungu kutoka mbinguni, wakati maji yanakuwa magumu kama jiwe, wakati uso wa vilindi vya maji unaganda? “Je, unaweza kuufunga mnyororo wa Kilimia? Unaweza kulegeza kamba za Orioni? Unaweza kuyaongoza makundi ya nyota kwa majira yake, au kuongoza Dubu na watoto wake? Je, unajua sheria zinazotawala mbingu? Unaweza kuweka utawala wa Mungu duniani? “Unaweza kuipaza sauti yako hadi mawinguni, na kujifunika mwenyewe na gharika ya maji? Je, wewe hutuma miali ya radi kwenye njia zake? Je, hutoa taarifa kwako kukuambia, ‘Sisi tuko hapa’? Ni nani aliyeujalia moyo hekima au kuzipa akili ufahamu? Nani mwenye hekima ya kuyahesabu mawingu? Ni nani awezaye kuinamisha magudulia ya mbinguni mavumbi yanapokuwa magumu, na mabonge ya udongo kushikamana pamoja?