Ayubu 38:1-11
Ayubu 38:1-11 NENO
Kisha Mwenyezi Mungu akamjibu Ayubu kutoka upepo wa kisulisuli. Akasema: “Nani huyu atiaye mashauri yangu giza kwa maneno yasiyo na maarifa? Jikaze kama mwanaume; nitakuuliza swali, nawe unijibu. “Ulikuwa wapi nilipoweka misingi ya dunia? Niambie, kama unafahamu. Ni nani aliyeweka alama vipimo vyake? Hakika wewe unajua! Ni nani aliyenyoosha kamba ya kupimia juu yake? Je, misingi yake iliwekwa juu ya nini, au ni nani aliyeweka jiwe la pembeni, wakati nyota za asubuhi zilipoimba pamoja, na malaika wote walipokuwa wakishangilia kwa furaha? “Ni nani aliyeifungia bahari milango ilipopasuka kutoka tumbo, nilipoyafanya mawingu kuwa vazi lake, na kuyafungia katika giza nene, nilipoamuru mipaka yake, na kuiweka milango yake na makomeo mahali pake, niliposema, ‘Unaweza kufika hapa, wala si zaidi; hapa ndipo mawimbi yako yenye kiburi yatakapokomea’?