Yohana 7:1-9
Yohana 7:1-9 NENO
Baada ya mambo haya, Isa alienda sehemu mbalimbali za Galilaya. Hakutaka kwenda Yudea kwa sababu viongozi wa Wayahudi huko walitaka kumuua. Sikukuu ya Vibanda ya Wayahudi ilikuwa imekaribia. Hivyo ndugu zake Isa wakamwambia, “Ondoka hapa uende Yudea ili wanafunzi Wako wapate kuona miujiza unayofanya. Mtu anayetaka kujulikana hafanyi mambo yake kwa siri. Kama unafanya mambo haya, jioneshe kwa ulimwengu.” Hata ndugu zake mwenyewe hawakumwamini. Isa akawaambia, “Wakati wangu bado haujawadia, lakini wakati wenu upo siku zote. Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi, lakini unanichukia mimi kwa sababu ninawashuhudia kwamba matendo yao ni maovu. Ninyi nendeni kwenye Sikukuu, lakini mimi sitahudhuria Sikukuu hii kwa sababu wakati wangu haujawadia.” Baada ya kusema hayo, akabaki Galilaya.