Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yohana 3:30-36

Yohana 3:30-36 NEN

Yeye hana budi kuwa mkuu zaidi na mimi nizidi kuwa mdogo.” “Yeye ajaye kutoka juu yu juu ya yote, yeye aliye wa duniani ni wa dunia, naye huzungumza mambo ya duniani. Yeye aliyekuja kutoka mbinguni, yu juu ya yote. Yeye hushuhudia yale aliyoyaona na kuyasikia, lakini hakuna yeyote anayekubali ushuhuda wake. Lakini yeyote anayekubali huo ushuhuda anathibitisha kwamba, Mungu ni kweli. Yeye aliyetumwa na Mungu husema maneno ya Mungu, kwa kuwa Mungu humtoa Roho pasipo kipimo. Baba anampenda Mwana, naye ametia vitu vyote mikononi mwake. Yeyote anayemwamini Mwana ana uzima wa milele, lakini yeye asiyemwamini Mwana hatauona uzima, bali ghadhabu ya Mungu itakuwa juu yake.”

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Yohana 3:30-36