Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia Utangulizi

Utangulizi
Kitabu hiki kimepewa jina la Yeremia, mwana wa kuhani, aliyezaliwa katika kijiji cha Anathothi. Kinatoa taarifa kwa kina na mtazamo wa kidini, na hali ya kisiasa katika Yuda kwenye kipindi cha miaka arobaini kabla ya kuharibiwa kwa Yerusalemu. Mengi yanajulikana kuhusu historia binafsi ya Yeremia kuliko nabii mwingine yeyote katika Manabii. Yeremia, kama Isaya, alikuwa kijana aliyeitwa na Mwenyezi Mungu kuionya Yuda juu ya uovu wake.
Kwa miaka ishirini na moja ya kwanza ya huduma ya Yeremia, taifa la Yuda, chini ya utawala wa Yosia, lilipata mwamko wa kisiasa na uamsho wa kiroho; wakati huo dola ya Waashuru ilikuwa inadidimia. Yeremia alipoanza huduma yake ya unabii 627 K.K., alikuwa na muda mzuri wa huduma hadi Yosia alipouawa mnamo 609 K.K.
Baada ya Yosia kuuawa, Yeremia alikuwa katika hatari kubwa kutoka kwa viongozi wa dini na wa kisiasa ambao walikasirishwa na ujumbe wake. Ingawa Yeremia alishauri Wayahudi wajitolee kwa Wababeli, wao waliasi. Hivyo mnamo mwaka wa 586 K.K., mji wa Yerusalemu pamoja na Hekalu lake vikaharibiwa, naye Yeremia akachukuliwa kwa nguvu na watu wa Yuda, wakaenda naye Misri licha yake kuwaonya wasiende, akafia huko.
Mwandishi
Nabii Yeremia.
Kusudi
Yeremia anatoa wito kwa Waisraeli kuacha dhambi na kumrudia Mwenyezi Mungu.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
Mnamo 627–586 K.K.
Wahusika Wakuu
Wafalme wa Yuda: Yosia, Yehoahazi, Yehoyakimu, Yehoyakini na Sedekia; Yeremia, Baruku, Ebed-Meleki, Mfalme Nebukadneza na viongozi wake, Warekabi, na watu wa Yerusalemu na Yuda.
Wazo Kuu
Uovu usipotubiwa husababisha taifa, jamii, au mtu binafsi kuangamia.
Mambo Muhimu
Yeremia aliorodhesha dhambi za Yuda zote na kutoa unabii wa hukumu ya Mwenyezi Mungu, na pia kuwaita watu watubu. Lakini watu waliendelea na maisha yao ya ubinafsi na kuabudu sanamu. Pia, viongozi wote walikataa Torati ya Mwenyezi Mungu, wakakubaliana na manabii wa uongo. Yerusalemu iliharibiwa, Hekalu likaachwa likiwa magofu, nao watu wakatekwa na kupelekwa uhamishoni Babeli. Iliwapasa watu kuwajibika kwa ajili ya uharibifu na utekwaji huu uliosababishwa na wao kutokusikia na kutokutii ujumbe wa Mwenyezi Mungu.
Yaliyomo
Wito wa Yeremia (1:1-19)
Hali ya dhambi ya Israeli na Yuda (2:1–6:30)
Kuasi Mwenyezi Mungu na kuvunja agano lake (7:1–12:17)
Uhakika wa kutekwa (13:1–18:23)
Yeremia akabiliana na viongozi (19:1–29:32)
Kurejeshwa na kufanywa upya (30:1–33:26)
Ufalme unasambaratika (34:1–39:18)
Watu wakimbilia Misri (40:1–45:5)
Jumbe kuhusu mataifa ya kigeni (46:1–51:64)
Kuanguka kwa Yerusalemu (52:1-34).

Iliyochaguliwa sasa

Yeremia Utangulizi: NENO

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia