Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 22:13-19

Yeremia 22:13-19 NEN

“Ole wake yeye ajengaye jumba lake la kifalme kwa njia ya dhuluma, vyumba vyake vya juu kwa udhalimu, akiwatumikisha watu wa nchi yake pasipo malipo, bila kuwalipa kwa utumishi wao. Asema, ‘Nitajijengea jumba kuu la kifalme, na vyumba vya juu vyenye nafasi kubwa.’ Hivyo anaweka ndani yake madirisha makubwa, huweka kuta za mbao za mierezi, na kuipamba kwa rangi nyekundu. “Je, inakufanya kuwa mfalme huko kuongeza idadi ya mierezi? Je, baba yako hakuwa na chakula na kinywaji? Alifanya yaliyo sawa na haki, hivyo yeye akafanikiwa katika yote. Aliwatetea maskini na wahitaji, hivyo yeye akafanikiwa katika yote. Je, hiyo si ndiyo maana ya kunijua mimi?” asema BWANA. “Lakini macho yako na moyo wako vimeelekezwa tu katika mapato ya udhalimu, kwa kumwaga damu isiyo na hatia, kwa uonevu na ukatili.” Kwa hiyo hili ndilo asemalo BWANA kuhusu Yehoyakimu mwana wa Yosia mfalme wa Yuda: “Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, ndugu yangu! Ole, umbu langu!’ Hawatamwombolezea wakisema: ‘Ole, bwana wangu! Ole, fahari yake!’ Atazikwa maziko ya punda: ataburutwa na kutupwa nje ya malango ya Yerusalemu.”