Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Yeremia 2:11-13

Yeremia 2:11-13 NEN

Je, taifa limebadili miungu yake wakati wowote? (Hata ingawa hao si miungu kamwe.) Lakini watu wangu wamebadili Utukufu wao kwa sanamu zisizofaa kitu. Shangaeni katika hili, ee mbingu, nanyi tetemekeni kwa hofu kuu,” asema BWANA. “Watu wangu wametenda dhambi mbili: Wameniacha mimi, niliye chemchemi ya maji yaliyo hai, nao wamejichimbia visima vyao wenyewe, visima vilivyobomoka, visivyoweza kuhifadhi maji.