Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waamuzi 6:12-16

Waamuzi 6:12-16 NEN

Malaika wa BWANA alipomtokea Gideoni, akamwambia, “BWANA yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.” Gideoni akajibu, “Ee Bwana wangu, kama BWANA yu pamoja nasi, mbona mambo haya yote yametutokea? Yako wapi basi yale matendo yake makuu baba zetu waliyotusimulia juu yake waliposema, ‘Je, BWANA hakutupandisha kutoka Misri?’ Lakini sasa BWANA ametuacha na kututia katika mkono wa Midiani.” BWANA akamgeukia na kusema “Enenda kwa uwezo wako huu, ukawaokoe Israeli kutoka mikononi mwa Wamidiani. Je, si mimi ninayekutuma wewe?” Gideoni akauliza, “Ee Bwana wangu, nitawezaje kuwaokoa Israeli? Ukoo wangu ndio dhaifu kuliko zote katika Manase, nami ndiye mdogo wa wote katika jamaa yangu.” BWANA akamjibu, “Nitakuwa pamoja nawe, nawe utawapiga Wamidiani kana kwamba walikuwa ni mtu mmoja.”