Waamuzi 6:11-12
Waamuzi 6:11-12 NEN
Malaika wa BWANA akaja akaketi chini ya mti wa mwaloni huko Ofra, ambao ulikuwa mali ya Yoashi, Mwabiezeri, ambako Gideoni mwanawe alikuwa akipepeta ngano penye shinikizo la kukamulia zabibu, ili kuificha Wamidiani wasiione. Malaika wa BWANA alipomtokea Gideoni, akamwambia, “BWANA yu pamoja nawe, Ewe shujaa mwenye nguvu.”