Isaya 9:4-7
Isaya 9:4-7 NENO
Kama vile siku ya kushindwa kwa Wamidiani, umevunja nira iliyowalemea, ile gongo mabegani mwao na fimbo ya aliyewadhulumu. Kila kiatu cha shujaa kilichotumiwa vitani, na kila vazi lililovingirishwa katika damu vitawekwa kwa ajili ya kuchomwa, vitakuwa kuni za kuwasha moto. Kwa maana, kwa ajili yetu mtoto amezaliwa, tumepewa mtoto wa kiume, nao utawala utakuwa begani mwake. Naye ataitwa Mshauri wa Ajabu, Mungu Mwenye Nguvu, Baba wa Milele, Mfalme wa Amani. Kuongezeka kwa utawala wake na amani hakutakuwa na mwisho. Atatawala kwenye kiti cha utawala cha Daudi na juu ya ufalme wake, akiuthibitisha na kuutegemeza kwa haki na kwa adili, tangu wakati huo na hata milele. Wivu wa Mwenyezi Mungu, Mungu wa majeshi ya mbinguni utatimiza haya.