Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 7:10-17

Isaya 7:10-17 NEN

BWANA akasema na Ahazi tena, “Mwombe BWANA Mungu wako ishara, iwe kwenye vina virefu sana, au kwenye vimo virefu sana.” Lakini Ahazi akasema, “Sitaomba; sitamjaribu BWANA.” Ndipo Isaya akasema, “Sikia sasa, ewe nyumba ya Daudi! Je, haitoshi kujaribu uvumilivu wa wanadamu? Je, mtaujaribu uvumilivu wa Mungu wangu pia? Kwa hiyo Bwana mwenyewe atawapa ishara: Bikira atachukua mimba, naye atamzaa mwana, na ataitwa Imanueli. Atakula jibini na asali atakapokuwa ameweza kukataa mabaya na kuchagua mema. Lakini kabla mtoto hajajua kukataa mabaya na kuchagua mema, nchi ya wafalme hao wawili unaowaogopa itafanywa ukiwa. BWANA ataleta juu yako, juu ya watu wako, na juu ya nyumba ya baba yako wakati ambao haujawahi kuwako tangu Efraimu alipojitenga na Yuda: yeye atawaleteeni mfalme wa Ashuru.”

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha