Isaya 55:8-11
Isaya 55:8-11 NENO
“Kwa kuwa mawazo yangu si mawazo yenu, wala njia zenu si njia zangu,” asema Mwenyezi Mungu. “Kama vile mbingu zilivyo juu kuliko dunia, ndivyo njia zangu zilivyo juu kuliko njia zenu na mawazo yangu kuliko mawazo yenu. Kama vile mvua na theluji ishukavyo kutoka mbinguni, nayo hairudi tena huko bila kunywesha dunia na kuichipusha na kuistawisha, ili itoe mbegu kwa mpanzi na mkate kwa mlaji, ndivyo lilivyo neno langu litokalo kinywani mwangu: Halitanirudia tupu, bali litatimiliza lile nililokusudia, na litafanikiwa katika kusudi lile nililolituma.