Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Isaya 41:13-17

Isaya 41:13-17 NEN

Kwa maana Mimi ndimi BWANA, Mungu wako, nikushikaye mkono wako wa kuume na kukuambia, Usiwe na hofu, nitakusaidia. Usiogope, ee Yakobo uliye mdudu, ee Israeli uliye mdogo, kwa kuwa Mimi mwenyewe nitakusaidia,” asema BWANA, Mkombozi wako, yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. “Tazama, nitakufanya chombo cha kupuria, kipya na chenye makali, chenye meno mengi. Utaipura milima na kuiponda na kuvifanya vilima kuwa kama makapi. Utaipepeta, nao upepo utaichukua, dhoruba itaipeperushia mbali. Bali wewe utajifurahisha katika BWANA na katika utukufu wa yeye Aliye Mtakatifu wa Israeli. “Maskini na wahitaji wanatafuta maji, lakini hayapo, ndimi zao zimekauka kwa kiu. Lakini Mimi BWANA nitawajibu, Mimi, Mungu wa Israeli, sitawaacha.

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha