Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Waebrania 7:11-17

Waebrania 7:11-17 NENO

Kama ukamilifu ungeweza kupatikana kupitia kwa ukuhani wa Walawi (kwa kuwa katika msingi huo, sheria ilitolewa kwa watu), kwa nini basi kulikuwa na haja ya kuja kuhani mwingine: kuhani kwa mfano wa Melkizedeki, wala si kwa mfano wa Haruni? Kwa kuwa ukuhani ukibadilika, lazima sheria nayo ibadilike. Yeye ambaye mambo haya yanasemwa alikuwa wa kabila lingine, na hakuna mtu wa kabila hilo aliyewahi kuhudumu katika madhabahu. Kwa maana ni dhahiri kwamba Bwana wetu alitoka katika uzao wa Yuda, tena kuhusu kabila hilo Musa hakusema lolote kwa habari za makuhani. Tena hayo tuliyosema yako wazi zaidi kama akitokea kuhani mwingine kama Melkizedeki, yeye ambaye amefanyika kuhani si kwa misingi ya sheria kama ilivyokuwa kwa baba zake, bali kwa misingi ya uwezo wa uzima usioharibika. Kwa maana imeshuhudiwa kwamba: “Wewe ni kuhani milele, kwa mfano wa Melkizedeki.”