Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Hagai Utangulizi

Utangulizi
Hagai ni moja ya vitabu vitatu vya kinabii vya Agano la Kale vilivyoandikwa baada ya uhamisho. Hagai na Zekaria ndio waliowatia moyo watu waliorudi kutoka uhamishoni kujenga upya Hekalu baada ya Mfalme Dario kupitisha amri kuwaruhusu Wayahudi kurudi Yerusalemu.
Kundi la kwanza la Wayahudi liliporudi Yerusalemu liliweka msingi wa Hekalu jipya wakiwa na furaha na matumaini makubwa. Hata hivyo, Wasamaria na majirani wengine walipinga ujenzi huo kwa nguvu nyingi na kuwakatisha tamaa wafanyakazi, na hata kuufanya ujenzi huo usimame. Watu wakageukia ujenzi wa nyumba zao wenyewe. Ujumbe wa Hagai ulikuwa kwamba ni wakati wa kujenga nyumba ya Mungu.
Mwandishi
Hagai.
Kusudi
Kuwahimiza watu kujenga upya Hekalu la Bwana, na kuwahamasisha kuyatengeneza maisha yao upya na Mungu ili waweze kupata baraka zake.
Mahali
Yerusalemu.
Tarehe
520 K.K.
Wahusika Wakuu
Hagai, Zerubabeli, Yoshua.
Wazo Kuu
Hagai aliwaambia watu kwamba utukufu wa Hekalu walilokuwa wanajenga ungekuwa mkubwa kuliko ule wa Hekalu lililotangulia, ingawaje halingekuwa imara kama la kwanza. Hili Hekalu lingekuwa bora zaidi kwa sababu Mungu angelijaza utukufu wake ndani yake.
Mambo Muhimu
Kuwaita watu kujenga upya Hekalu la Yerusalemu lililobomolewa, na ahadi ya Mungu ya kuwabariki kama wangemtii.
Mgawanyo
Wito wa kujenga Hekalu (1:1-15)
Matumaini ya Hekalu jipya (2:1-9)
Baraka zilizoahidiwa (2:10-19)
Ushindi wa mwisho wa Mungu (2:20-23).

Iliyochaguliwa sasa

Hagai Utangulizi: NEN

Kuonyesha

Shirikisha

Nakili

None

Je, ungependa vivutio vyako vihifadhiwe kwenye vifaa vyako vyote? Jisajili au ingia

YouVersion hutumia vidakuzi kubinafsisha matumizi yako. Kwa kutumia tovuti yetu, unakubali matumizi yetu ya vidakuzi kama ilivyoelezwa katika Sera yetu ya Faragha