Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Habakuki 1:12-17

Habakuki 1:12-17 NEN

Ee BWANA, je, wewe sio wa tangu milele? Mungu wangu, Uliye Mtakatifu wangu, hatutakufa. Ee BWANA, umewachagua wao ili watekeleze hukumu; Ee Mwamba, umewaamuru watuadhibu. Macho yako ni safi mno hata yasiweze kuutazama uovu, wala huwezi kuvumilia makosa. Kwa nini basi unawavumilia wadanganyifu? Kwa nini unakuwa kimya wakati waovu wanawameza wale wenye haki kuliko wao wenyewe? Umewafanya watu kama samaki baharini, kama viumbe wa bahari wasio na mtawala. Adui mwovu anawavuta wote kwa ndoana, anawakamata katika wavu wake, anawakusanya katika juya lake; kwa hiyo anashangilia na anafurahi. Kwa hiyo anatoa kafara kwa wavu wake, na kuchoma uvumba kwa juya lake, kwa kuwa kwa wavu wake anaishi kwa starehe, na anafurahia chakula kizuri. Je, aendelee kuwatoa walio katika wavu wake, akiangamiza mataifa bila huruma?