Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 29:28-35

Mwanzo 29:28-35 NENO

Naye Yakobo akafanya hivyo. Akamaliza juma na Lea, kisha Labani akampa Raheli binti yake kuwa mke wake. Labani akamtoa Bilha mjakazi wake kwa Raheli ili kuwa mtumishi wake. Pia Yakobo akakutana na Raheli kimwili, naye akampenda Raheli kuliko Lea. Yakobo akamtumikia Labani kwa miaka mingine saba. Mwenyezi Mungu alipoona kwamba Lea hapendwi, akamwezesha kupata watoto, lakini Raheli alikuwa tasa. Lea akapata mimba, akazaa mwana. Akamwita jina Reubeni, kwa maana alisema, “Ni kwa sababu Mwenyezi Mungu ameona huzuni yangu. Hakika mume wangu sasa atanipenda.” Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Kwa sababu Mwenyezi Mungu alisikia kwamba sipendwi, amenipa tena huyu mwana.” Kwa hiyo akamwita jina Simeoni. Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Sasa mume wangu ataambatana na mimi, kwa sababu nimemzalia wana watatu.” Kwa hiyo akamwita jina Lawi. Akapata tena mimba, naye alipozaa mwana akasema, “Wakati huu nitamsifu Mwenyezi Mungu.” Kwa hiyo akamwita jina Yuda. Kisha akaacha kuzaa watoto.