Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 28:12-15

Mwanzo 28:12-15 NENO

Akaota ndoto, na katika ndoto hiyo aliona ngazi imesimamishwa juu ya ardhi, ncha yake ikiwa imefika mbinguni. Nao malaika wa Mungu walikuwa wakipanda na kushuka kwa ngazi hiyo. Juu yake alisimama Mwenyezi Mungu, akasema, “Mimi ni Mwenyezi Mungu, Mungu wa baba yako Ibrahimu, na Mungu wa Isaka. Nchi ambayo umelala juu yake, nitakupa wewe na uzao wako. Uzao wako utakuwa kama mavumbi ya nchi, nawe utaenea upande wa magharibi na mashariki, kaskazini na kusini. Kupitia wewe na uzao wako, mataifa yote ya duniani yatabarikiwa. Niko pamoja nawe, nami nitakulinda popote utakapoenda, na nitakurudisha katika nchi hii. Sitakuacha hadi nitakapofanya hayo niliyokuahidi.”