Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Mwanzo 12:4-9

Mwanzo 12:4-9 NEN

Hivyo Abramu akaondoka kama BWANA alivyokuwa amemwambia; naye Loti akaondoka pamoja naye. Wakati Abramu alipoitwa aondoke Harani, alikuwa na miaka sabini na mitano. Abramu akamchukua Sarai mkewe pamoja na Loti mwana wa ndugu yake, mali zote walizokuwa nazo pamoja na watu aliokuwa amewapata huko Harani, wakasafiri mpaka nchi ya Kanaani, wakafika huko. Abramu akasafiri katika nchi hiyo akafika huko Shekemu, mahali penye mti wa mwaloni ulioko More. Wakati huo Wakanaani walikuwa wanaishi katika nchi hiyo. BWANA akamtokea Abramu, akamwambia, “Nitawapa uzao wako nchi hii.” Hivyo hapa akamjengea madhabahu BWANA aliyekuwa amemtokea. Kutoka huko Abramu akasafiri kuelekea kwenye vilima mashariki ya Betheli, naye akapiga hema huko, Betheli ikiwa upande wa magharibi na Ai upande wa mashariki. Huko alimjengea BWANA madhabahu na akaliitia jina la BWANA. Kisha Abramu akasafiri kuelekea upande wa Negebu.

Mipango ya Kusoma Bila Malipo na Ibada zinazohusiana na Mwanzo 12:4-9